English:

By signing this registration form to participate in the Bagamoyo Historical Marathon (‘the Event’) the entrant and participant accept the following;- 

Precautions have been taken by the organizing body to ensure safety of all participants, however there may be dangers inherent in the participation or activities associated with the event, thus participants assume the risk of attendance and participation and waive all claims of any nature that arise in relation suppliers and assistants of these parties including any individual, official, marshal, or agent (‘the parties’) 

Participant to the Event indemnify and hold harmless the parties against liabilities that shall arise from delay, inconvenience, accident, death, injury, illness to their persons, loss or damage to property or costs and expenses sustained, incurred or put to by participants and/ or by any minor children under the care under the care under control of Participants. 

Participants acknowledge this is the public event and therefore give permission for the free use of his/ her name, voice, still and moving picture to be used in any broadcast, telecast, advertising, promotion, or any other form of advertising of this or future events. 

Parents/ Guardian authorizing minor to participate in the Event must sign this registration from which shall imply that they have consented such minor being bound to all terms and conditions for this event and further indemnify the Parties to the extent, if any, to which such minor is not capable of waiving his/her rights as stipulated herein.

 

Kiswahili: 

Kwa kusaini hii fomu ya kujiunga na Bagamoyo Historical Marathon (‘Tukio’), mshiriki anakubali na kuridhia yafuatayo:-

  1. Pamoja nakwamba waandaaji wamechukua tahadhari zote kuhakikisha usalama wa Washiriki ajali na hatari zinaweza kutokea, hivyo washiriki kwa ridhaa yao wenyewe wanaafiki kushiriki katika mashindano haya wakitambua uwezekano wa hatari na ajali kutokea na kwa ajili hiyo wanatoa kinga ya kutodai fidia au madai ya aina yoyote pamoja na Wakurugenzi, Wagavi na wasaidizi wao wote waliotajwa hapa, pamoja na mtu binafsi, Afisa au Wakala (‘Wahusika’) 
  1. Mshiriki wa Tukio anatoa kinga na anaahidi kutodai fidia wala madai ya aina yoyote yale iwe yamesababishwa moja kwa moja au la, iwe imesababishwa kwa uzembe au la, au kwa kushiriki au kuhusika katika kupita njia au kwa tukio au kwa namna nyingine ikijumuisha ucheleshaji, usumbufu, ajali, kifo, kuumia, Ugonjwa kwa watu wao, au hasara au uharibifu kwenye mali au gharama na matumizi yaliyofanyika, kufanyika au kuwekwa na Washiriki na/au mtu yeyote Yule Chini ya uangalizi au usimamizi wa washiriki. 
  1. Mshiriki anathibitisha kuwa na uwezo kiafya na kiakili na ana Mamlaka ya kusaini hii fomu ya usajili na kukubaliana na masharti haya.
  2. Mshiriki ninatoa ruhusa na ridhaa ya kutumia pasipo malipo au madai ya aina yoyote, jina langu, sauti, picha yangu inayosimama na inayotembea, itumike katika matangazo, mawasiliano ya aina yoyote ile ya matangazo ya sasa na kwa matukio ya baadae. 
  1. Mzazi/Msimamizi wanao waruhusu watoto kushiriki ni lazima wasaini fomu hii na itamaanisha kukubalika na kuafki kuwa mtoto atashiriki kwa masharti na vigezo, vya tukio hili, na aidha kwa Wahusika kwa kiwango, iwapo kipo, ambacho mtoto hataweza kuondoa haki na madai yake kama yalivyoelezwa humu